Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AASILI MTOTO MCHANGA ALIYEOKOLEWA NZEGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike leo, 11 Machi 2026, katika makazi yake ya Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mtoto huyo, aliyepewa jina Grace Samia Suluhu Hassan, alitelekezwa mjini Nzega, mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Dkt. Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Mhe. Naitapwaki Tukai.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mtoto, Mkuu wa Wilaya Tukai amesema Grace alikimbizwa Januari 17, 2026, akiwa ametelekezwa karibu na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini. Baada ya kupokea taarifa, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua mtoto na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiwa hazina mafanikio.

Rais Dkt. Samia amemkaribisha mtoto huyo katika familia yake na kuahidi kumpatia malezi, ulinzi, na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni bora kumkabidhi mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto ni hazina, hatuijui kesho yake,” amesema Rais Dkt. Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com