Hatua ya Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzisha mchakato wa mtaala maalumu wa teknolojia ya uzalishaji kuku nchini, ni zaidi ya mpango wa elimu; ni ufunguo wa kiuchumi kwa vijana wa Kitanzania.
Tamko la Naibu Waziri, Ng’wasi Kamani, lililotolewa Machi 23, 2026, linaashiria mwisho wa ufugaji wa mazoea na mwanzo wa tasnia inayojiendesha kisayansi.
Kwa kijana anayetafuta fursa, mtaala huu wa Astashahada na Stashahada unamaanisha kuwa soko la ajira sasa linakwenda kuhitaji "madaktari wa kuku" na wabobezi wa teknolojia ya kitalu, hatua inayopandisha hadhi ya mfugaji kutoka mtu wa hali ya chini hadi mtaalamu msimamizi wa uchumi wa mabilioni.
Maana ya maamuzi haya katika mnyororo wa thamani ni mapinduzi kuanzia kwa mzalishaji wa vifaranga, mtengeneza chakula cha mifugo, hadi kwa mlaji wa mwisho.
Kuwapo kwa wataalamu wabobezi kutaondoa hasara za vifo vya kuku zinazotokana na ukosefu wa utaalamu, hivyo kupunguza gharama za uzalishaji na kufanya bei ya kuku na mayai kuwa nafuu na yenye ubora kwa mlaji hasa ikizingatiwa kwamba ulaji wa nyama ya kuku kitaifa ni asilimia 18.
Hali hiyo inatengeneza mzunguko wa fedha wenye tija ambapo mfugaji anapata faida kubwa, na viwanda vya kusindika nyama ya kuku vinapata malighafi ya uhakika, jambo linalochochea ukuaji wa viwanda vidogo na vya kati nchi nzima.
Kuhusu ajira na utekelezaji wa Ilani ya CCM (2020-2030), hatua hii ni jibu la moja kwa moja kwa ahadi ya kutengeneza fursa milioni nane za ajira. Serikali inatambua kuwa sekta ya mifugo ndiyo mwajiri mkuu wa vijana, na kwa kuanzisha mafunzo haya, inawaandaa vijana kuwa waajiri badala ya waajiriwa.
Huu ni utekelezaji wa vitendo wa ilani unaolenga kuongeza mchango wa sekta ya mifugo kwenye Pato la Taifa (GDP), huku ikihakikisha kuwa kuelekea uchaguzi wa 2030, vijana wengi watakuwa wamejikita katika miradi ya ujasiriamali iliyosukwa kitaalamu na yenye uhakika wa masoko ya ndani na nje ya nchi.
Tukiitazama Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, programu hii ni msingi wa Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati uliokomaa. Dira hiyo inalenga kuwa na Taifa lenye ushindani wa kimataifa, na teknolojia ya kuku ndiyo itakayotufanya tuwe kitovu cha usambazaji wa bidhaa za kuku katika soko la Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).
Kwa kuwekeza kwenye "akili" (mtaala), serikali inatayarisha kizazi kitakachotumia Akili Unde (AI) na mitambo ya kisasa kusimamia mashamba makubwa ya kuku, hali itakayohakikisha usalama wa chakula na lishe kwa miaka 25 ijayo, huku ikiondoa umaskini wa kipato kwa kaya za vijana.
Kwa kijana wa Kitanzania, huu ni wito wa kuchangamkia fursa. Serikali imeshafungua njia kwa kukusanya maoni kutoka sekta binafsi ili kuhakikisha mafunzo haya yanashabihiana na mahitaji ya soko la kweli la kibiashara.
Huu si wakati wa kusubiri ajira za ofisini, bali ni wakati wa kuingia darasani kupata utaalamu wa teknolojia ya kuku na kisha kuingia mtaani kumiliki mnyororo wa thamani. Serikali ya Awamu ya Sita imeshaweka mazingira wezeshi; sasa ni zamu ya vijana kugeuza mtaala huu kuwa utajiri wa kijani na nyeupe, kuelekea maisha bora na yenye tija katika uchumi wa
Social Plugin