Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA 2026, KUFANYIKA BUSANDA- SHINYANGA, WADAU WAKARIBISHWA

Na Mwandishi Wetu

Maonesho ya Mifugo Kanda ya Ziwa (Lakezone Livestock Expo) yanatarajia kufanyika Mei 30-31 mwaka huu, Busanda Mkoani Shinyanga, ambapo wadau mbalimbali wa mifugo wanatarajiwa, kushiriki.

Kwa mujibu wa Diana Lukio Ambaye ni Mwandaaji wa maonesho hayo, amebainisha kuwa, yatawakutanisha wafugaji, wakulima na wadau wote kwenye mnyororo wa thamani kutoka Mikoa ya Shinyanga, Mara, Simiyu, Mwanza, Geita, Tabora na Kagera.

"Ni maonesho ya kihistoria ambayo yatakuwa na vitu vingi vya kujifunza juu ya ufugaji wa kisasa, masoko, fedha, bima za mifugo, breeds and feeds za kisasa. 

"Karibu tujifunze na kuwekeza kwenye ufugaji biashara", amesema Diana Lukio.

Aidha, kwa washiriki ama udhamini wanaweza kuwasilisha moja kwa moja na waandaji kwa namba +255762918153 

Ambapo kwa sasa hatua za awali zinaendelea za maonesho hayo.

Maonesho hayo ya mifugo Kanda ya Ziwa, ambapo yanaenda kwa kauli mbiu: "Ufugaji Biashara" pia yataambatana na mabanda mbalimbali ya wadau, huku kukiwa na shughuli za minada, maonesho, biashara ya bidhaa mbalimbali za mifugo na wadau na Ngoma za Asili.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com