Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. YONAZI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA TACAIDS


Na maandishi wetu,Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Adam Joseph Mrisho ambaye amefika kujitambulisha baada ya kuteuliwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 23 Machi, 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo mtaa wa Reli jijini Dodoma na kudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. James Kilabuko pamoja na Mratibu wa Masuala ya UKIMWI  Adela Mpina.

Dkt.Yonazi ameahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com