Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO, (Msumbiji), Ndugu Chakil Felizardo Passadas Aboobacar, ambaye ameanza ziara rasmi ya kikazi kwa siku mbili nchini.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 6 Machi 2026, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar Es Salaam, vyama hivyo viwili ambavyo vina urafiki na udugu wa kihistoria, vimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili, hasa kushirikiana kiuchumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com