
Na Mwandishi Wetu
Wakati wengine wakizani kuwa na "kitambi" au mwili nyumba ni ishara ya maisha mazuri, Wizara ya Afya imepuliza filimbi ya hatari! Takwimu mpya zinaonesha kuwa kasi ya Watanzania kuongezeka unene uliopitiliza inatisha, na sasa tumefika asilimia 30 kutoka asilimia 26 ya awali.
Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa Yasiyoambukiza, Dk. Omary Ubuguyu, ameweka wazi kuwa huku si kuteleza, bali ni kuanguka kwenye mtego wa magonjwa yasiyoambukiza.
Habari Njema na Habari Mbaya:
Tumeshinda hapa: Matumizi ya tumbaku yameshuka (14% hadi 9%), pombe imepungua (29% hadi 19%), na ulaji wa mboga za majani umeanza kushika kasi.
Tumefeli hapa: Licha ya juhudi zote, eneo la unene uliopitiliza limebaki kuwa "miba" inayotuchoma.
Dk. Ubuguyu anasema, wakati vifo vya magonjwa haya Afrika Mashariki ni 41%, Tanzania tupo kwenye 34%. Lakini hatuwezi kubweteka! Mpango mkakati mpya wa nchi za ukanda huu unakuja na "nguvu ya pamoja"—ikiwemo kuweka sheria kali za kuzuia bidhaa hatari zinazoingizwa sokoni na kushusha gharama za dawa.
Social Plugin