Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI BARRICK BULYANHULU WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUWAPA FARAJA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUPAMBA

Wafanyakazi Wanawake wa Barrick Bulyanhulu wakigawa zawadi mbalimbali na kuwafariji watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Bupamba iliyopo halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani

Wafanyakazi Wanawake na Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Afisa Elimu wa Kata ya Kharumwa, Aloyce Masse akisoma risala ya shukrani kwa wafanyakazi wanawake wa Barrick Bulyanhulu walipotembelea shule ya msingi Bupamba katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick Bulyanhulu wakigawa zawadi mbalimbali na kuwafariji watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Bupamba iliyopo halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick Bulyanhulu wakigawa zawadi mbalimbali na kuwafariji watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Bupamba iliyopo halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Wafanyakazi Wanawake na Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja baada ya kutembelea shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Bupamba iliyopo halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

***

Katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani 2026, wafanyakazi wanawake wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu wametembelea shule ya msingi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Bupamba iliyopo halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita ambapo wamewapelekea zawadi mbalimbali.

Akiongea kuhusu tukio hilo, Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bi. Mary Lupamba amesema ziara hiyo ni sehemu ya utamaduni wa mgodi huo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambapo wafanyakazi wanawake hutumia siku hiyo kuwafikia wadau mbalimbali katika jamii na kutoa msaada wa kijamii kama ishara ya mshikamano na upendo.

“Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Kampuni inatumia siku hii kama jukwaa la kutathmini na kuendeleza juhudi za wanawake kazini, kusaidia jamii zinayozunguka migodi hususani makundi yenye mahitaji maalum kama haya na kushiriki katika program Kuchochea wanawake kuingia katika mnyororo wa sekta ya madini”,amesema Lupamba.

Naye Kiongozi wa msafara wa wafanyakazi hao Bi. Asmina Matinga akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi za msaada kwa uongozi wa shule hiyo kuwa wafanyakazi wanawake wa mgodi huo wameona umuhimu wa kusherehekea siku hiyo kwa vitendo kwa kuwafikia watoto wenye mahitaji maalum.

Amesema watoto wenye mahitaji maalum wanastahili kupendwa, kuthaminiwa na kupewa fursa sawa kama ilivyo kwa watoto wengine katika jamii “Kuja kwetu kuwatembelea ni ishara ya kuonesha kwamba jamii inatambua haki zenu na mnpaswa kujiamini ili muweze kutimiza ndoto zenu za maisha”, amesisitiza.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Kata ya Kharumwa, Aloyce Masse, amesema Halmashauri kupitia Idara ya Elimu Msingi iliona umuhimu wa kuwaweka pamoja wanafunzi wenye changamoto za kimaumbile kama vile kuona, kusikia, kuongea na wenye changamoto za ngozi ili kurahisisha utoaji wa msaada na huduma maalum kwao.

Masse kwa niaba ya shule ya msingi Bupamba ametoa shukrani kwa Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu kwa hatua hiyo ya kuwafariji watoto hao, akisema msaada waliotoa unaleta faraja kubwa na kuwapa hamasa wanafunzi hao kuendelea kusoma kwa bidii na kujiona ni sehemu ya jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com