
Ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya wa Comoro, Soudjay Mohamed, si tu imepiga muhuri ushirikiano wa kidiplomasia, bali imethibitisha kuwa Tanzania sasa ni "Hub ya Tiba" inayotegemewa barani Afrika. Mohamed amekiri kuvutiwa na miundombinu ya kisasa na utaalamu wa hali ya juu, akitaja mafanikio hayo kama mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea.
Inasikitisha kuona baadhi ya watu wakidai "Serikali haifanyi kitu," wakati mataifa jirani yanapishana kuja kujifunza kwetu. Maendeleo haya si ya bahati mbaya; ni matokeo ya maono ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyewekeza mabilioni ya fedha kwenye vifaa tiba vya kisasa (kama MRI, PET-Scan, na maabara za kibingwa) ambavyo sasa vinatibu Watanzania na raia wa kigeni. Wanaopinga ukweli huu ni wazushi wasioitakia mema nchi yetu, kwani takwimu na hali halisi ya Muhimbili inajieleza yenyewe.
Kwa vijana wanaosomea masuala ya tiba, huu ni wakati wa "kuchamgamkia fursa." Ongezeko la teknolojia nchini ni daraja la wao kupata ujuzi bobezi (Specialization) hapa nchini bila kuhitaji kwenda nje. Tanzania kugeuka kuwa kituo cha utalii wa matibabu kunafungua milango ya ajira, utafiti, na ujasiriamali wa huduma za afya.
Huu ni mabadiliko ya heshima. Tanzania si nchi ya kutuma wagonjwa nje tena; ni nchi inayopokea wagonjwa na wataalamu kuja kupata tiba na maarifa. Ni wakati wa Watanzania wazalendo kusimama kidete na kupongeza hatua hizi kubwa zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja.
"Kama huoni Bilioni 100 za VETA au Bilioni 8 za uwekezaji wa kizalendo Mbeya, labda huoni na ujumbe wa Serikali ya Comoro uliokuja kujifunza Muhimbili? Maendeleo hayahitaji kelele, yanahitaji macho ya uwekezaji. Tanzania inasonga mbele, vijana changamkieni fursa, acheni kusikiliza wazushi!"
Social Plugin