Kupitia mitandao ya kijamii kunasambazwa picha mjongeo akionekana mtoto mdogo wa kiume na zikisikika sauti zikimhamasisha kuvuta sigara Kitendo hicho ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za kijamii na nchi. Jeshi la Polisi, limeanza uchunguzi na kuwafuatilia watu hao kwa hatua nyingine za kisheria.
Aidha, linatoa wito kwa yeyote anayewafahamu watu hao au mtoto huyo atusaidie kuwafikia na kuokoa afya ya mtoto huyo.
Pia, linatoa onyo kwa watu wenye tabia za kufanya vitendo vya kikatili na vya unyanyasaji kama hivyo na vinavyofanana na hivyo kwa watoto kwa lengo lolote lile ikiwepo msukumo wa kutafuta wafuasi (followers) kwa ajili ya mitandao yao ya kijamii kuziacha kwani halitasita kuwakamata kwa sababu ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Social Plugin