Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UJUMBE WA BARAZA LA ELIMU YA JUU AFRIKA MASHARIKI (IUCEA) UMEFANYA ZIARA KATIKA CHUO CHA VETA-BURUGO KAGERA




Na Mbuke Shilagi Kagera. 

Ujumbe wa Baraza la Elimu ya Juu Afrika Mashariki (IUCEA) umefanya ziara katika chuo cha Veta kilichopo Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera Februari 12,2026.

Akizungumza mara baada ya kutembelea karakana, Mawa Michael ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa Taasisi inayosimamia Elimu ya Juu Afrika Mashariki  inayojumuisha Nchi nane amesema kuwa wamevutiwa na ubora wa vifaa vya kisasa vinavyotumika kufundishia katika chuo hicho.

Aidha amebainisha kuwa wametembelea karakana za umeme, ufundi sanaa na uchomeleaji, na kutoa wito kwa Nchi wanachama kuongeza uwekezaji kwa vijana kama ambavyo Tanzania imefanya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA, Abdallah Ngodu, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa VETA katika ziara ya Taasisi inayosimamia Elimu ya Juu Afrika Mashariki walipotembelea Chuo cha Ufundi na Huduma mkoani Kagera amesema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) nchini, imepanga kuanzisha mafunzo maalum kwa wajasiriamali wadogo ili kuwajengea uwezo wa kutumia vyema fursa za biashara na kujikwamua kiuchumi pamoja na kukuza mitaji yao.

Aidha amesema mpango huo unalenga kuwafikia wadau wa sekta isiyo rasmi wakiwemo mama lishe, wauzaji wa batiki na wafugaji wa samaki kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kila kundi ili kuwawezesha kuongeza tija katika shughuli zao.

Awali, Mkuu wa Chuo hicho, Maganga Kashinje, akitoa taarifa, amebainisha kuwa Chuo kinatoa fani saba na kina uwezo wa kudahili wanafunzi 1,000 kwa mwaka.


Ujumbe wa Baraza la Elimu ya Juu Afrika Mashariki na Viongozi mbalimbali wa VETA Tanzania

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com