Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAKWIMU ZAZUNGUMZA: SHINYANGA MANISPAA KINARA WA UFAULU SHULE ZA MSINGI,WALIMU WAKABIDHIWA TUZO

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akikabidhi tuzo na vyeti kwa shule ambazo zimefanya vizuri kwenye masomo ,mtihani wa darasa la nne na la saba.
Na Stella Herman,Shinyanga

Manispaa ya Shinyanga imeshika  nafasi ya kwanza Kimkoa kati ya halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga  Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba (PSLE) mwaka 2025, kwa kupata asilimia 87 ya ufaulu wa jumla hatua ambayo inafanya kuendelea kung’ara.

Akizungumza na walimu katika hafla ya kukabidhi tuzo kwa shule zilizofanya vizuri zikiwemo za serikali na binafsi, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amewapongeza walimu pamoja na Idara ya Elimu ya Awali na Msingi kwa ubunifu wa kutoa motisha kwa walimu wanaofanya vizuri.

Ameeleza kuwa walimu wanapaswa  kujifunza kutoka shule zilizofanya vizuri zaidi na kubadilishana uzoefu na mbinu bora za ufundishaji ili kuimarisha ubunifu na ubora wa elimu Hatua hiyo itasaidia kuinua zaidi viwango vya elimu ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Mafanikio hayo yameitambulisha Manispaa hiyo kama kinara wa ubora wa elimu ya msingi, yakionesha dhamira thabiti ya kuinua viwango vya elimu kwa vitendo,kupitia shule za serikali na shule binafsi.

Kufuatia matokeo  mazuri, idara ya Elimu ya Awali na Msingi  Manispaa ya Shinyanga imeandaa hafla maalum ya kutunuku vyeti vya pongezi kwa walimu pamoja na shule za msingi zilizofanya vizuri Mtihani wa Darasa la Saba (PSLE) 2025 na Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA) 2025

Hatua hiyo imelenga kutambua mchango wa walimu na kuhamasisha juhudi zaidi katika kuinua taaluma ili kuleta tija zaidi

.Kazi ya kukabidhi tuzo inaendelea kwa shule mbalimbali binafsi na za serikali

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Revocatus Lutunda

Hatua hiyo imelenga kutambua mchango wa walimu na kuhamasisha juhudi zaidi katika kuinua taaluma ili kuleta tija zaidi.

Akitoa taarifa ya matokeo hayo, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi Manispaa ya Shinyanga, Mary Samson Maka, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa karibu kati ya walimu, wanafunzi, wazazi na wasimamizi wa elimu.

Amesema  mshikamano huo umewezesha kuwepo kwa mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia, hali iliyochangia ufaulu mkubwa.

Amesema Manispaa ya Shinyanga pia imeibuka ya kwanza kimkoa katika Mtihani wa Upimaji Darasa la Nne (SFNA) kwa kupata asilimia 82.25 ya ufaulu wa jumla matokeo hayo yanaonesha msingi imara wa elimu ya awali na mwelekeo chanya wa maendeleo ya elimu ya msingi kuanzia ngazi za chini.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Revocatus Lutunda, amesema walimu ni nguzo muhimu ya maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla.

Amepongeza bidii na moyo wa kujituma wa walimu, akibainisha kuwa mafanikio hayo ni uthibitisho kuwa uwekezaji katika elimu una matokeo chanya ya muda mrefu.



 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com