Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MTOTO MTANZANIA ASAJILIWA CELTA VIGO SPAIN

 

Habari njema kwa Watanzania, Joseph Jr Michael (JJ), amepiga hatua kubwa baada ya kusajiliwa na klabu ya Celta Vigo nchini Hispania kwenye timu ya vijana (Juvenil B) kupitia dirisha dogo la usajili Januari 2026. 

JJ mwenye umri wa miaka 18  anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati, amejiunga akitokea Shule ya Mpira wa Miguu ya Denis Suárez Fernández. Katika msimu wa 2024–2025, alicheza mechi 12 katika ligi ya Preferente Futgal Juvenil, akionyesha uchezaji wa kiwango cha juu na uimara katika ulinzi. 

Beki huyo wa kati kutoka Tanzania pia ana uzoefu wa kimataifa, akiwa amewahi kufanya mafunzo na kucheza katika akademi ya Celta Vigo  nchini Hispania, Usajili wake  unaongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya kikosi hicho.

Hii ni fahari kwa familia, Akademi yake ya nyumbani  Magnet Youth academy na Tanzania kwa ujumla. Ni ushahidi kwamba ndoto za vijana wa Kitanzania zinatimia, na Tanzania inazidi kung'ara kimataifa kwenye Michezo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com