Dar es Salaam imepokea mgeni wa kipekee, Meli ya Crystal Symphony. Hii si meli tu, ni kama mji mzima ulioshushwa majini ukiwa na watalii 522 na wahudumu 492, tayari kumwaga neema nchini, jamii hiyo imekuja kutalii.
Amani, utulivu uliopo na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan yameifanya bandari yetu kuwa shamba linaloweza kupokea mavitu ya kitalii. Ujio wa meli hiyo ni ishara nyingine kubwa ya kuonesha umuhimu wa amani na mafanikio makubwa ya serikali ya awamu ya sita katika uboreshaji wa miundiombinu inayowezesha watalii wanaozunguka na meli za kifahari kututembelea.
Ujio wa meli hii ni simulizi tosha ya mabadiliko ya kifikira kwa vijana nini wafanye kwani serikali imewekeza katika mazingira sahihi ya kufungua fursa mbalimbali za vijana wanaoshughulika na utalii na mafanikio yao ni kuwezesha mzunguko mzima wa fedha kitaani.
Wakati watalii hawa wanashuka kutembelea vivutio vya asili na kihistoria, wanatafuta mikono ya vijana wabunifu na wakifanbikiwa mazungumzo na watu wa kwao wanafanya Tanzania kuendelea kuwa kituo muhimu cha meli za kifahari zinazozunguka duniani na watalii.
Uwepo wa bidhaa za kipekee na huduma bora zinayohitajika ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja kunafanya vijanba wa Dar es salaam kutengeneza huduma mbalimbali zitakazowafanya watalii hawa kuwa na kumbukumbu ya kutosha nzuri kuhusu Tanzania.
Bandari kama Lango la Mapinduzi na kupitia filamu ya The Royal Tour, dunia sasa inaitazama Tanzania kama sehemu ya lazima kufika.
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Abed Gallus Abed, anathibitisha kuwa huduma zimeboreshwa na sasa hata meli kubwa zaidi zinaweza kutia nanga kwa urahisi kwa sababu ya kuongezwa kwa kina cha maji na kuboreshwa kwa gati.
Kama anavyosema John Ndauka wa Inchcape Shipping Services, miundombinu imeshaandaliwa; kilichobaki ni vijana kuchangamkia fursa hizi kwa akili na ubunifu kwani sasa nmilango ya utajiri imefunguka kupitia bandari yetu.

Social Plugin