Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAFISA UDAHILI NA MAAFISA MITIHANI KUTOKA VYUO MBALIMBALI TANZANIA WAENDELEA KUPIGWA MSASA SHINYANGA



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mafunzo maalum ya Maafisa Udahili na Maafisa Mitihani yanayoendeshwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yameendelea leo Februari 5, 2026 katika Ukumbi wa NSSF, Manispaa ya Shinyanga, huku washiriki wakijadili na kupokea mada mbalimbali zinazolenga kuboresha mifumo ya udahili na mitihani katika vyuo vya elimu ya ufundi nchini.

Katika siku ya pili ya mafunzo hayo, washiriki wameendelea kuwasilishwa mada zinazohusu matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki ya NACTVET, taratibu za udahili wa wanafunzi, usimamizi wa mitihani pamoja na upakiaji wa matokeo kwa kuzingatia miongozo na kalenda ya kitaaluma ya Baraza.

Mada hizo zimejikita katika kuimarisha ufanisi wa utekelezaji wa majukumu ya Maafisa Udahili na Mitihani, kupunguza changamoto za ucheleweshaji wa taarifa katika kanzidata ya Baraza pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma kwa wakati ikiwemo mikopo, vyeti na fursa za ajira.

Washiriki kutoka vyuo mbalimbali nchini wamepata fursa ya kujadili kwa vitendo changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kubadilishana uzoefu kuhusu namna bora ya kuzitatua kwa kuzingatia miongozo ya NACTVET.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kufikia tamati leo, yakiwa na matarajio ya kuongeza ufanisi katika udahili na mitihani, kuboresha utoaji wa huduma kwa wanafunzi na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Soma pia : NACTVET YAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA UDAHILI NA MITIHANI KUIMARISHA UFANISI WA MIFUMO VYUONI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com