Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akihutubia wana CCM na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini katika mkutano uliofanyika Februari 22, 2026 kwenye Ukumbi wa Ukumbi wa Lyakale akisisitiza mshikamano, uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa maendeleo ya wananchi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akihutubia wanaCCM na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini katika mkutano uliofanyika Februari 22, 2026 kwenye Ukumbi wa Ukumbi wa Lyakale.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Patrobas Katambi, amewashukuru wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga na viongozi wa Serikali kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kusimamia uchaguzi na kuhakikisha ushindi wa madiwani, wabunge na Rais unapatikana kwa kishindo.
Akizungumza katika Ukumbi wa Lyakale Mjini Shinyanga mbele ya wana CCM na viongozi wa CCM kutoka kata zote za wilaya hiyo, Katambi amesema amekuja rasmi kutoa shukrani kwa wananchi kwa imani waliyoionesha kwake na kwa chama.
"Lengo la kuja kwenu ni kuwashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya, hivyo niwaahidi tutasimamia miradi yote ya maendeleo, na nitasimamia haki zote za wananchi, na niwahakikishie sitamuonea mtu, kwani tunataka haki kwa sababu tunasimamia misingi ya kikatiba."
Amesema ushindi huo umetokana na umoja, mshikamano na kazi kubwa iliyofanywa na wananchi pamoja na viongozi wa CCM katika kuhamasisha upigaji kura na kuhakikisha chama kinapata kura nyingi za kishindo.
Katambi ameahidi kuendeleza ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni na kusisitiza kuwa maendeleo yatabaki kuwa ajenda kuu ya uongozi wake.
"Tutaendelea kutoa huduma kwa wananchi kama tulivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi", amesema Katambi.
Ameeleza kuwa yeye pamoja na madiwani na wabunge wenzake wana wajibu wa kusimamia miradi yote ya maendeleo, akibainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
"Mimi na viongozi wenzangu madiwani wabunge ni jukumu letu kuwaletea maendeleo, na kusimamia miradi yote ya maendeleo, Rais Samia Suluhu ameleta fedha nyingi hivyo niwaombe wakandarasi waliopewa dhamana ya kufanya kazi wafanye kazi kwa wakati, sitakubaliana na mkandarasi ambaye atachelewesha kazi bila sababu maalumu", amesema Katambi.
Katambi amesema Serikali itaendelea kuboresha miradi na huduma katika sekta zote kwa lengo la kuhakikisha maendeleo endelevu yanafikiwa.
"Ipo miradi endelevu tutaendelea kuboresha, sekta kwa sekta tutaendelea kuziboresha", amesema Katambi.
Katika kusisitiza utawala wa haki na misingi ya kikatiba, Katambi amesema hatamwonea mtu yeyote na atasimamia haki kwa wote bila upendeleo.
Kuhusu amani na usalama wa nchi, Katambi amesema Shinyanga itaendelea kuwa salama kwa sababu Tanzania ni nchi yenye amani, akisisitiza kuwa maendeleo hayawezi kupatikana pasipo utulivu.
"Shinyanga itaendelea kuwa salama kwa sababu nchi ina amani, huwezi kufanya shughuli za maendeleo kama hakuna amani", amesema.
Ameongeza kuwa hali ya usalama nchini ni tulivu huku Serikali ikiendelea kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
"Tunaendelea kukabiliana na changamoto ndogo ndogo, hakuna tukio kubwa baya, hakuna tukio la tishio la usalama wa nchi", amesema.
Amesema kwa sasa aina mpya ya uhalifu imehamia zaidi mtandaoni na kwamba wizara yake imeelekeza nguvu katika kukabiliana na vitendo hivyo ili kulinda taswira ya nchi.
"Uhalifu mkubwa sasa hivi upo mtandaoni, wapo watu wanaotukana mtandaoni, wanatoa matamshu ya uongo, ulaghai, utapeli. Tunataka kuona usalama wa nchi unakuwa salama. Hivi sasa tumeelekeza nguvu mtandaoni kwa sababu huko kuna uhalifu, anayechafua nchi tutamfuata huko huko aliko", ameongeza Katambi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ukweli katika siasa na taasisi za kidini.
"Pia tutahakikisha siasa za ukweli, ukweli katika taasisi za kidini", ameeleza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, amewataka wananchi na viongozi wa chama kuendelea kumpa ushirikiano na kumuombea Katambi kutokana na uzito wa wizara anayoiongoza.
"Niwaombe wananchi na viongozi wa CCM tuendelee kumpa ushirikiano kijana wetu ili aendelee kupiga kazi, niwaombe muendelee kumwamini kijana huyu, kwa upendo mliouonyesha wa kumpigia kura nyingi naamini atafanya kazi kubwa, ila nafasi hii tuendelee kuiombea aendelee kuisimamia vizuri."
Ameongeza kuwa baada ya uchaguzi, wanachama wanapaswa kuachana na majungu na kuelekeza nguvu katika kuijenga Shinyanga na Taifa kwa ujumla.
"Pia niwaombe tuache ushabiki wa majungu kwa sababu uchaguzi tumemaliza kinachotakiwa, tusitumie muda mwingi kumshauri majungu tutumie muda wetu kumshauri kuleta maendeleo ya Shinyanga na Taifa la nchi yetu tuachane na wapambe nuksi tuwe wapambe wa maendeleo muda wa kampeni umeisha tuwe pamoja kwani CCM ni moja, hivyo tuendelee kulinda amani yetu ya Tanzania", ameeleza.
ANGALIA PICHA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akihutubia Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini katika mkutano uliofanyika Februari 22, 2026 kwenye Ukumbi wa Ukumbi wa Lyakale akisisitiza mshikamano, uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu kwa maendeleo ya wananchi. Picha zote na Kadama Malunde
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akizungumza na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akizungumza na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akizungumza na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akizungumza na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akizungumza na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, akizungumza na Viongozi wa CCM Jimbo la Shinyanga Mjini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog



































































































Social Plugin