Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MBONI MHITA ATOA MAELEKEZO MAZITO KUIMARISHA ULINZI WA BARABARA, AIPONGEZA TANROADS NA TARURA KWA KAZI KUBWA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.

Na  Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amesisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi, akitaka usimamizi mkali wa barabara na uwajibikaji wa viongozi katika ngazi zote. 

Akizungumza Februari 24, 2026 wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhita amesema pamoja na changamoto za kibajeti na athari za mabadiliko ya tabianchi, barabara nyingi zimeendelea kupitika mwaka mzima, jambo linalodhihirisha dhamira thabiti ya Serikali katika kuhakikisha miundombinu inakuwa endelevu.

Amesema Serikali inaendelea kuelekeza rasilimali katika ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), hatua ambayo imeongeza upatikanaji wa huduma za kijamii na kurahisisha usafirishaji wa mazao na bidhaa.

Ameeleza kuwa kikao hicho cha kwanza kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kimefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007, na ni jukwaa muhimu la kutathmini hali ya barabara, kupanga mikakati na kuweka vipaumbele vya maendeleo ya mkoa.

“Kikao hiki kinatuwezesha kujadili kwa kina maendeleo ya Mkoa wetu na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha sekta ya barabara kwa manufaa ya wananchi,” amesema Mhita.
Katika kuimarisha usimamizi wa miundombinu, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa maelekezo kadhaa, ikiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri kutekeleza maelekezo ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI ya kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya TARURA kwa halmashauri zinazokusanya zaidi ya shilingi bilioni tano.

Maelekezo mengine ni pamoja na kusimamia kikamilifu sheria za uzito wa magari ili kulinda ubora na uimara wa barabara, kuandaa na kutekeleza mikakati ya matengenezo kinga pamoja na matengenezo ya dharura, hasa katika kipindi cha mvua na kudhibiti uvamizi wa hifadhi za barabara na biashara zisizo rasmi zinazofanyika katika maeneo hayo.

Aidha, amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu hiyo, akisisitiza kuwa jukumu la kuitunza ni la kila mmoja kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

APONGEZA JUHUDI ZA TANROADS NA TARURA

Mhita amepongeza kazi inayofanywa na TANROADS na TARURA katika kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote, ikiwemo kufungua mitaro na kuboresha mifereji ya maji ili kupunguza athari za mafuriko, hususan katika Manispaa za Shinyanga na Kahama.
“Hongereni sana TANROADS na TARURA kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kusimamia miundombinu ya barabara,” amesema Mhe. Mhita.

Pamoja na mafanikio hayo, ametaja changamoto zinazoendelea kuikabili sekta hiyo, ikiwemo uvamizi wa hifadhi za barabara, mifugo kuzurura barabarani, utupaji holela wa taka kwenye mitaro pamoja na baadhi ya wakandarasi kukosa uwezo wa kutekeleza miradi kwa viwango vinavyotakiwa.

Ameagiza mamlaka husika kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria ndogo ndogo ili kulinda uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya miundombinu.

Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa barabara ni mhimili wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kwamba ushirikiano wa wadau wote ni muhimu kuhakikisha miundombinu hiyo inadumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wabunge wa Mkoa wa Shinyanga, ambapo Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hilal Hamad, ameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kuimarisha usalama na hadhi ya barabara. Mhe. Azza ameiomba Serikali kuweka taa za barabarani katika njiapanda ya Tinde na Didia pamoja na kufunga taa za kuongozea magari katika njiapanda ya Tinde, ili kupunguza hatari kutokana na ongezeko la magari na watembea kwa miguu. 

Aidha, ameomba barabara ya Didia–Solwa kupandishwa hadhi ili kuhudumu kwa kiwango kinachostahili, sambamba na kuwekewa lami kipande cha barabara kutoka njiapanda ya Didia (Puni) hadi Didia Senta ambapo kuna reli ya SGR kwa lengo la kurahisisha usafiri, usafirishaji wa mazao na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga Februari 24,2026
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga Februari 24,2026
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga Februari 24,2026
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati akifungua Kikao cha Bodi ya Barabara mkoa wa Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com