Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIMARISHA MKAKATI DHIDI YA TEMBO WAHARIBIFU HANDENI



Na mwandishi wetu, Dodoma.

Serikali imesema imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Utatuzi wa Migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori, kwa lengo la kulinda maisha ya wananchi na mali zao katika maeneo yanayoathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu, ikiwemo Wilaya ya Handeni.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Hamad Chande wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Handeni, Charles Jacob Sungura, aliyehoji mkakati wa Serikali wa kutatua changamoto ya tembo wanaoharibu mazao na kuhatarisha maisha ya wananchi katika maeneo ya Mzeli, Sindeni na Kwamatuku.

Akijibu, Naibu Waziri amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali mahsusi katika maeneo hayo ili kupunguza migongano kati ya binadamu na wanyamapori, huku ikihakikisha usalama wa wananchi unaimarishwa.

Ameeleza kuwa miongoni mwa hatua zilizotekelezwa ni kuanzishwa kwa kituo cha kudumu cha Askari Wanyamapori katika eneo la Handeni, hatua inayolenga kuongeza mwitikio wa haraka pale matukio ya uvamizi wa tembo yanapotokea pamoja na kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com