Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAELEZA SABABU ZA KUTOWALAZIMISHA WATOTO KUWAHUDUMIA WAZAZI



Na Jackline Minja MJJWM-Dodoma

Serikali imesema haina haja ya kuweka sharti la kisheria linalowalazimisha watoto kuwahudumia wazazi wao wasiojiweza, ikieleza kuwa suala hilo tayari linashughulikiwa kupitia misingi ya kifamilia na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa kinondoni Mhe. Tarimba Gulam Abbas lililohoji "Je Serikali haioni haja ya kuweka sharti la kisheria la watoto wakubwa kutunza wazazi wao wasiojiweza"

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali inatambua umuhimu wa familia na jamii katika kuchukua jukumu la kulea na kuwahudumia wazee, akisisitiza kuwa huo ni msingi wa mila na desturi za Watanzania.

Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuimarisha huduma na matunzo kwa wazee kupitia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003, Toleo la mwaka 2024, ambayo inasisitiza wajibu wa familia na jamii katika kuwahudumia wazee wao.

Hata hivyo, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha maadili ya uwajibikaji wa kifamilia na kuimarisha mifumo ya kijamii inayosaidia ustawi wa wazee nchini.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com