Mhandisi Ujenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Aikande Munuo, akitoa elimu kuhusu ishara na alama za barabarani zitakazowekwa katika maeneo ya utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limehitimisha zoezi la utoaji elimu kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) kutoka Dar es Salaam hadi Isaka, unaotarajiwa kuanza rasmi Aprili 2026 na kukamilika mwaka 2029.
Zoezi hilo lililoanza Julai 2025 limehitimishwa Januari 29, 2026 katika Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, likilenga kuwajengea uelewa wananchi wanaopitiwa na mradi kuhusu fursa za kiuchumi, tahadhari za usalama na wajibu wa kushirikiana na TRC wakati wa utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati.
Akizungumza wakati wa hitimisho la zoezi hilo, Mhandisi Ujenzi wa TRC, Aikande Munuo, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanza rasmi Awamu ya Pili ya Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati, unaolenga kuhuisha reli ya zamani, kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na abiria, pamoja na kuimarisha uchumi wa taifa kwa kuiweka Bandari ya Nchi Kavu ya Isaka katika nafasi ya kimkakati ya usafirishaji wa kikanda.
Amesema kupitia mradi huo, Serikali imepokea Dola za Marekani milioni 200 (takribani Shilingi bilioni 500) kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya reli ya kati, uwekezaji unaolenga kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Mhandisi Aikande ameongeza kuwa Awamu ya Kwanza ya mradi ilitekelezwa kuanzia mwaka 2017 hadi 2022, lakini haikuweza kukamilisha malengo yote kutokana na upungufu wa rasilimali fedha. Katika awamu hii ya pili, TRC itatekeleza kazi kubwa ikiwemo utandikaji wa reli kwa umbali wa kilomita 392.4 kutoka Dar es Salaam hadi Isaka, ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga kazi zitajikita zaidi katika kipande cha Tabora–Isaka.
Ameeleza kuwa reli zote chakavu zitaondolewa na kuwekwa reli mpya, nzito na zenye uwezo wa kupitisha treni ndefu na mizigo mizito zaidi, hatua itakayopunguza gharama za usafirishaji, kuongeza usalama na kuifanya Isaka kuwa lango kuu la mizigo kwa nchi jirani za Kanda ya Kati na Maziwa Makuu.
“Mradi huu unalenga kuongeza usalama wa usafiri wa reli, kupunguza gharama za usafirishaji, kukuza biashara, ajira na kuchochea maendeleo katika maeneo yanayopitiwa na reli. Isaka ni kituo muhimu cha usafirishaji, na ukarabati huu utaifanya Bandari Kavu ya Isaka kuwa kitovu kikubwa zaidi cha uchumi na biashara za kikanda,” amesema Mhandisi Aikande.
Ameongeza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo, TRC inashirikiana kwa ukaribu na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) ili kuhakikisha uwekezaji huo unaleta manufaa mapana zaidi kwa wananchi. Kupitia ushirikiano huo, madaraja 171 yatakarabatiwa na kuongezewa uwezo wa kupitisha maji ili kuondoa changamoto za mafuriko, sambamba na ujenzi na ukarabati wa mabwawa sita kwa ajili ya kuboresha usimamizi wa maji na kuunga mkono shughuli za kilimo.
Kuhusu manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi, Mhandisi Aikande amesema mradi huo utafungua fursa za ajira, hususan ajira za muda wakati wa ujenzi na ukarabati wa reli, pamoja na kuongeza shughuli za kibiashara kutokana na usafirishaji rahisi wa mazao, bidhaa na mizigo kwa gharama nafuu.
Wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, wakisoma vipeperushi vya elimu kuhusu Mradi wa TIRP II
Aidha, mradi huo utaimarisha usafiri wa haraka na salama, kuchochea ukuaji wa mji wa Isaka, na kuvutia uwekezaji zaidi katika maeneo ya karibu na reli ikiwemo ujenzi wa maghala, masoko na huduma nyingine za kijamii na kibiashara.
Kwa upande wake, Mhandisi wa TRC, Justine Kalokola, amewahimiza wananchi kuzingatia tahadhari za usalama karibu na reli, kuepuka kukaa, kucheza au kupita kiholela katika njia ya reli, pamoja na kufuata alama na maelekezo yatakayotolewa wakati wa utekelezaji wa mradi.
Mwanasheria wa TRC, Jane Kassanda, amewakumbusha wananchi kuwa ni kosa kisheria kuharibu au kuiba miundombinu ya reli, pamoja na kuweka vizuizi kwenye njia ya reli, akisisitiza umuhimu wa kuepuka vitendo vya rushwa na uharibifu vinavyoweza kusababisha ajali na hasara kubwa kwa taifa.
Naye Afisa Jamii wa TRC, Lightness Mngulu, amefafanua kuwa mradi huo utaleta manufaa makubwa kwa jamii, ikiwemo upatikanaji wa ajira za moja kwa moja na kuongezeka kwa fursa za wananchi kujiongezea kipato kupitia biashara zao kutokana na ongezeko la watu katika Kata ya Isaka.
Hata hivyo, amebainisha pia uwepo wa changamoto zinazoweza kujitokeza, zikiwemo uchafuzi wa mazingira pamoja na mmomonyoko wa maadili.
Kwa upande wake, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Adija Salimu, amesema mafanikio ya mradi yanategemea ushirikiano kati ya TRC na wananchi, akiwahimiza wananchi kulinda miundombinu ya reli na kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya hatari.
Diwani wa Kata ya Isaka, Mheshimiwa Pazi Majuto Pazi, amesema mradi huo ni fursa adhimu kwa maendeleo ya Isaka na Wilaya ya Kahama kwa ujumla, akiwataka wananchi kushirikiana kikamilifu na wadau wa mradi, kulinda miundombinu ya reli kama mali ya taifa na kutumia ipasavyo fursa zitakazojitokeza.
Mhandisi Ujenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Aikande Munuo, akitoa elimu kuhusu ishara na alama za barabarani zitakazowekwa katika maeneo ya utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.
Mhandisi Ujenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Aikande Munuo, akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.

Wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, wakisikiliza elimu kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka, iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Afisa Jamii wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Lightness Mngulu akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kuhusu fursa wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.

Mwanasheria wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jane Kassanda, akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kuhusu sheria na kanuni mbalimbali zinazolinda miundombinu ya reli.

Mwananchi akiuliza swali wakati Mwanasheria wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jane Kassanda, akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kuhusu sheria na kanuni mbalimbali zinazolinda miundombinu ya reli.
Mhandisi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Justine Kalokola akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kuhusu usalama wa miundombinu ya reli.
Mhandisi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Justine Kalokola akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kuhusu usalama wa miundombinu ya reli. Kulia ni Mhandisi Ujenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Aikande Munuo, akionesha ishara na alama za barabarani zitakazowekwa katika maeneo ya utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.
Mhandisi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Justine Kalokola akitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, kuhusu usalama wa miundombinu ya reli. Kulia ni Mhandisi Ujenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Aikande Munuo, akionesha ishara na alama za barabarani zitakazowekwa katika maeneo ya utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.
Wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, wakisikiliza elimu kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka, iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Adija Salimu, akitoa elimu kuhusu usalama na namna ya kulinda miundombinu ya reli.

Diwani wa Kata ya Isaka, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama, Mheshimiwa Pazi Majuto Pazi, akieleza namna wananchi wa Isaka walivyojipanga na kujiandaa kunufaika na fursa zitokanazo na utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.

Mkazi wa Isaka, Wilaya ya Kahama, akiuliza swali wakati Maafisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakitoa elimu kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.

Mwananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, akisoma vipeperushi vya elimu kuhusu Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.

Wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, wakisikiliza elimu kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka, iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, wakisikiliza elimu kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka, iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Mwananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, akisoma vipeperushi vya elimu kuhusu Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka.

Wananchi wa Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, wakisikiliza elimu kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Ukarabati wa Reli ya Kati Awamu ya Pili (TIRP II) unaoanzia Dar es Salaam hadi Isaka, iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Social Plugin