Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUANZISHA KITENGO MAALUM KUPOKEA MAONI YA WANANCHI SAA 24


Na. Mwandishi wetu - Rukwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu amesema Serikali itaanzisha kitengo maalum cha huduma kitakachofanya kazi kwa saa 24 chenye jukumu la kupokea, kusikiliza na kufanyia kazi maoni, mapendekezo pamoja na kero za wananchi.

Kitengo hicho kitawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja bila vikwazo vya kiurasimu na kusaidia Serikali kupata mrejesho wa haraka kwa ajili ya kuboresha sera na huduma.

Mhe. Sangu amebainisha hayo Disemba 23, 2025 Sumbawanga Mkoani Rukwa alipofanya kikao na wadau wa Mahusiano kutoka makundi ya Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na wawakilishi wa kundi la Vijana.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa mawasiliano na uwajibikaji kati ya Serikali na wananchi kwa ajili ya kuimarisha imani, mshikamano wa kitaifa na maendeleo jumuishi.

‎Aidha, amesema lengo la kikao ni kutambulisha shughuli za Ofisi yake na kutekekeza mkakati wa kuwafikia wadau wa mahusiano ili kujenga uelewa wa pamoja kwa maendeleo ya Taifa.

Kikao hicho kimeongozwa na Kauli mbiu isemayo "Mahusiano imara, Msingi wa Mshikamo wa Taifa"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com