
Meneja wa CRDB Bank Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza na walimu,wazazi na wanafunzi katika shule ya msingi Hanihani baada ya kukabidhi msaada wa madawati.

Na Stella Herman, Tabora
Katika mwendeleo wa kuhakikisha wanasaidia kupunguza changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu,CRDB Bank imetoa msaada wa madawati 40 kwa shule ya msingi Hanihani Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Akikabidhi madawati hay oleo Desemba 05,2025 Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wambura Wagana,amesema hatua hiyo inasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.
Amesema CRDB Bank inawajali wateja wake kwa kutoa misaada inayogusa Jamii ikiwa ni kurejesha sehemu ya faida yake kwa Jamii,kwa kuangalia changamoto zilizopo ili kusaidia kupeleka msaada.
“Tulipata maombi kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga kwamba kuna upungufu wa madawati kwa baadhi ya shule,na sisi kama wadau wa maendeleo tukaona tupeleeeke msaada hata kwa shule moja na tunafanya hivyo kupitia kampeni ya CRDB" keti jifunze" ambayo iko nchi nzima”amesema Wagana
Amewataka wanafunzi kuyatunza madawati hayo ili yaweze kudumu na kusaidia wengine kama wao walivyokuta madawati yaliyopo ambayo yalitunzwa na waliowatangulia kuanza kusoma.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Igunga Elizabeth Rwegasira ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga, ameishukuru CRDB kwa msaada wa madawati kwani umesaidia kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa chini ambapo wanafunzi 120 wanakaa chini.
Amesema CRDB Bank ni mdau mkubwa katika kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika sekta ya elimu,afya na mazingira,ambapo leo kupitia msaada wa madawati umesaidia kuwawezesha wanafunzi kuondokana na adha ya kusoma wakiwa wamekaa chini. 














Social Plugin