Na Maandishi wetu, DAR
Wananchi na Wafanyabiashara wa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar Es Salaam wameeleza kuwa kilichofanyika Oktoba 29, 2025 si maandamano bali ni uhalifu, uharibifu na wizi uliokuwa ukifanywa na magenge ya wahuni wachache, wakitaka hatua kali kuchukuliwa kwa wote watakaothibitika kujihusisha na magenge hayo.
Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania kulitokea vurugu na ghasia katika baadhi ya maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Songwe ambapo makundi ya Vijana yameonekana katika maeneo hayo, wakichoma, kuharibu na kuiba mali za umma na za watu binafsi ikiwemo uchomaji wa magari ya mwendokasi, wizi wa mafuta ya petroli na dizeli kwenye vituo vya uuzaji mafuta pamoja na uchomaji wa vituo vya uuzaji mafuta hayo.
"Kwanza sio desturi yetu kufanya maandamano na kimsingi yale hayakuwa maandamano kwasababu hawakuwa wakipaza ujumbe wowote kwa serikali, 'amesema mmoja wa mwanachi wa Dar


Social Plugin