Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE WA MONDULI "KADOGOO"AJA NA ARI MPYA KUMALIZA KERO ZA WANANCHI




Na Mwandishi wetu,Dodoma

Mbunge Mteule wa Monduli, Izack Joseph Copriano (Kadogoo), ashiriki kikao cha kwanza cha Bunge la 13 jijini Dodoma huku akiwa na Ari mpya kuwatumikia wakazi wa Monduli.

Izack Joseph Copriano, maarufu kama Kadogoo, Mbunge mteule wa Jimbo la Monduli (CCM), leo tarehe 11 Novemba 2025, ameshiriki kwa mara ya kwanza kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachoendelea jijini Dodoma.

Kikao hiki ni sehemu ya Bunge la 13, ambacho kimeanza leo na kujumuisha wabunge wapya pamoja na wale waliorejea, wakitarajiwa kuapa katika siku chache zijazo kabla ya kuanza rasmi majukumu yao.

 Kadogoo, ambaye kabla ya kugombea ubunge alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli alipata ushindi wake wa kishindo Oktoba 29, 2025, ameonekana akiwa na ari, nidhamu na hamasa kubwa ya kulitumikia Taifa, huku akisisitiza dhamira yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Monduli .

Katika kampeni zake, miongoni mwa ahadi zake zikizompa ushindi ni kutatua kero ya maji na kumaliza migogoro ya ardhi Monduli huku akiahidi kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya lakini pia suala la elimu likiwa kipaumbele kikubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com