
Ikiwa
imebaki siku moja kufika siku ya kupiga kura Oktoba 29, Umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa Shinyanga
umewaomba wananchi kutumia haki yao ya
kikatiba kwenda kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaowataka.
Hayo
yameelezwa leo Oktoba 27,2025 na Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa
Shinyanga Rashid Mohammed, wakati wakitoa tamko la kuwaomba wananchi wenye sifa
ya kupiga kura washiriki kikamilifu kupiga kura na kuwaomba wawapuuze watu
wanaotoa vitisho kwenye mitandao ya kijamii.
Viongozi hao
wamesema vyama vya siasa vimefanya kampeni zake kwa utulivu na amani hadi sasa wanaelekea siku ya uchaguzi na
kuwatoa hofu wananchi kuwa kuna amani ya kutosha na Shinyanga ni salama na
amani ipo ya kutosha.
Katika tamko la viongozi hao wameipongeza
serikali ya Mkoa kwa kushirikiana nao katika nyakati zote na kuchukuwa hatua
kutatua changamoto zilizokuwa zinajitokeza jambo ambalo limewapa faraja kubwa.
Mwenyekiti wa umoja wa vyama vya siasa Mkoa wa
Shinyanga Rashid Mohammed amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa nao sambamba
katika kuimarisha ulinzi na usalama hasa wakati wa kampeni zilizokuwa zikifanyika.
Viongozi hao
baada ya kutoa tamko lao pia wametumia fursa hiyo kunadi sera za vyama vyao na
kueleza mikakati yao,ambapo baadhi ya wagombea ubunge wametumia fursa hiyo
kuomba kura kwa wananchi ili wawachague Oktoba 29.



Baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa ambao pia ni wagombea ubunge

Social Plugin