Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : AZZA HILLAL AFUNGA KAMPENI KIBINGWA ITWANGI, MAELFU WAJITOKEZA MKUTANO MKUBWA FUNGA KAZI


@malundeblog

KISHINDO cha AZZA Hillal Akifunga KAMPENI Jimbo la ITWANGI! Aisee Tinde pamechangamka !

♬ original sound - Malunde

Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, amehitimisha kampeni zake kwa kishindo leo Oktoba 27, 2025, katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Kata ya Tinde, akiahidi kupigania maendeleo ya wananchi kwa vitendo mara baada ya kushinda uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

Mkutano huo umehudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM kutoka kata mbalimbali, ukiwa ni kilele cha kampeni za chama hicho katika jimbo hilo jipya, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa.

Akizungumza mbele ya umati mkubwa wa wananchi, Mhe. Azza Hillal Hamad ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo nchini, ikiwemo katika maeneo yanayounda Jimbo la Itwangi.

“Wananchi wa Itwangi, ninawashukuru kwa mapokezi yenu makubwa tangu nilipoanza kampeni. Dhamira yangu ni moja tu; kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wote. Tutahakikisha maji, barabara, elimu, afya na umeme vinaboreshwa zaidi. Nawaomba Oktoba 29 mjitokeze kwa wingi kunipigia kura mimi, Azza Hillal Hamad, pamoja na wagombea wote wa CCM hadi ngazi ya Urais,” amesema Azza.

Amesema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo jipya, atashirikiana kwa karibu na serikali katika kusukuma miradi muhimu ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji wa Tinde Package unaolenga kufikisha huduma ya maji kwa vijiji 18, ujenzi wa barabara na makavati, na kuboresha huduma za afya katika kila kata.

Aidha, Azza ametaja mafanikio yaliyokwisha kupatikana kupitia Serikali ya Awamu ya Sita kuwa ni pamoja na upatikanaji wa umeme katika vijiji vyote 58 vya Itwangi, ukamilishaji wa maboma ya zahanati, na kuboresha miundombinu ya shule.

“Mama Samia ni kiongozi jasiri na mwenye maono. Amefanya kazi kubwa sana katika kuwaletea Watanzania maendeleo. Ni wajibu wetu kumuunga mkono ili aendelee kutupeleka mbele,” ameongeza Azza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, amempongeza Azza Hillal Hamad kwa kampeni zake zenye mwelekeo wa maendeleo na moyo wa kujitolea kwa wananchi wake.

“Azza ni kiongozi mchapakazi, mwenye maono na anayegusa maisha ya wananchi. Tumpatie kura nyingi ili awe Mbunge wetu wa kwanza wa Jimbo la Itwangi na aendelee kushirikiana na Rais Dkt. Samia katika kuleta maendeleo zaidi,” amesema Mlolwa.

Mlolwa amewaasa wananchi wa Itwangi kujitokeza kwa wingi siku ya Oktoba 29 kupiga kura kwa amani, akisisitiza kuwa CCM ndiyo chama pekee kinachotekeleza ahadi zake na kuleta mageuzi chanya katika maisha ya Watanzania.

Kufungwa kwa kampeni hizo kunafungua ukurasa mpya wa historia katika Jimbo jipya la Itwangi, ambapo macho ya wengi yameelekezwa kwa Azza Hillal Hamad , mgombea anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa na aliyejipatia heshima kubwa kwa kujituma na kuonyesha dira ya kweli ya kiongozi anayewaza maendeleo ya wananchi wake.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, akielezea kwa wananchi namna sahihi ya kuwapigia kura wagombea wa CCM katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa (kulia) akielezea kwa wananchi namna sahihi ya kuwapigia kura wagombea wa CCM katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.
Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi kupitia CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi wa Itwangi.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025, ambapo aliwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura Oktoba 29.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akiomba kura wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025
Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, akiomba kura wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Kata ya Tinde, Oktoba 27, 2025.





@malundeblog WASWEZI noma sana! Tazama walivyoamsha amsha Azza Hillal akifunga Kampeni Jimbo la ITWANGI ♬ original sound - Malunde @malundeblog Mwanamke anayecheza na NYOKA Gumzo Tinde Azza Hillal akifunga Kampeni Jimbo la ITWANGI ♬ original sound - Malunde @malundeblog KISHINDO cha AZZA Hillal Akifunga KAMPENI Jimbo la ITWANGI! Aisee Tinde pamechangamka ! ♬ original sound - Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com