Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANESCO YAUNGA MKONO SEKTA YA AFYA KISHAPU, YATOA MASHUKA NA SABUNI WODI YA WAZAZI


Na Sumai Salum – Kishapu

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Shinyanga limetoa msaada wa mashuka na sabuni za kufulia kwa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Kishapu (Dr. Jakaya Mrisho Kikwete), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Oktoba 7, 2025, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Hussein Mbulu, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za shirika hilo kuunga mkono jamii na kuendelea kujenga matumaini kwa wagonjwa na wananchi kwa ujumla.

“Tumedhamiria kuwajali wagonjwa kwa kuwa wao pia ni wateja wetu. Tunaamini msaada huu utapunguza changamoto ya upungufu wa mashuka hospitalini na kuleta faraja kwa akina mama wanaohudumiwa,” amesema Mhandisi Mbulu.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Dkt. Charles Mlonganile, amewashukuru TANESCO kwa msaada huo na kueleza kuwa hospitali bado inahitaji mashuka na vifaa vingine muhimu vya utoaji huduma.

“TANESCO wameonesha mfano mzuri wa ushirikiano na jamii. Tunawaomba wadau wengine waendelee kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya,” amesema Dkt. Mlonganile.

Naye Muuguzi Kiongozi wa Idara ya Wazazi, Mwanahamisi Mohamed, amesema msaada huo umewatia moyo wauguzi kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wagonjwa, huku akisisitiza umuhimu wa wadau wengine kuiga mfano huo.

Kwa niaba ya akina mama wanaopatiwa huduma hospitalini hapo, Leah Charles, mkazi wa Idushi, ameipongeza na kuishukuru TANESCO kwa kuwakumbuka na kuwajali.

“Tumejiona kuthaminiwa sana. Tunawashukuru TANESCO kwa msaada huu ambao umetupa faraja kubwa, hasa sisi wazazi tunaohitaji mazingira safi na salama,” amesema Leah.Meneja wa TANESCO Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhandisi Hussein Mbulu akizungumza walipokuwa wakikabidhi msaada wa mashuka na sabuni za kufuria kwenye Wodi ya wazazi wanapoendelea na maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa wateja Hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani humo Oktoba 7,2025Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Dkt. Charles Mlonganile akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Shinyanga Oktoba 7,2025
Meneja wa TANESCO Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhandisi Hussein Mbulu(kushoto) na Mahasibu wa TANESCO mkoani Shinyanga Rebecca Kjigilia (kulia)
Muuguzi Kiongozi wa Idara ya Wazazi wa Hospitali ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Kishapu, Mwanahamisi Mohamed akizungumza baada ya kupokea msaada huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Shinyanga Oktoba 7,2025Mkazi wa Idushi Wilayani Kishapu Mkaoni Shinyanga Leah Charles

Baadhi ya Wafanyakzi kutoka Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoani Shinyanga na Wilayani Kishapu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada wa mashuka na sabuni za kufuria kwenye Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Dr.Jakaya Mrisho Kikwete ikiwa ni sehemu ya maaadhimisho ya Wiki ya huduma kwa wateja Oktoba 7,2025

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com