
Mgombea udiwani viti maalumu Wilaya ya Kishapu kupitia Kata ya Ukenyenge, Mhe. Sophia Masele, ameandaa bonanza la michezo katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukenyenge ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Katika bonanza hilo, lililofanyika Oktoba 5,2025 Mhe. Sophia Masele amemuwakilisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kishapu, Mh. Lucy Mayenga, ambapo amewaomba wananchi wa Kata ya Ukenyenge na wilaya nzima kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya urais, akisisitiza kuwa amefanya mageuzi makubwa ya kiuchumi na kusimamia vyema miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano inayomalizika.
Aidha, Mh. Masele amewaomba wananchi kumpa kura nyingi Mh. Lucy Mayenga kwa nafasi ya ubunge na pia kumchagua Mh. Anderson Mandia kwa nafasi ya udiwani.
Maelfu ya wananchi wamejitokeza kushiriki katika bonanza hilo ambapo michezo mbalimbali imefanyika, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha mshikamano, umoja na ushiriki wa pamoja kuelekea uchaguzi mkuu.

















Social Plugin