Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DR. ASHA - ROSE MIGIRO KATIBU MKUU CCM, ACHUKUA MIKOBA YA DKT. EMMANUEL NCHIMBI, KIHONGOSI MWENEZI!



Dkt. Asha-Rose Migiro ameteuliwa kumrithi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mgombea Mwenza wa urais wa Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025.
Uteuzi huo uliothibitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, yametangazwa mbele ya vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla mara baada ya kutangaza uteuzi wa mwisho wa wagombea ubunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi leo katika Ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Pia, Makalla amechukua fursa hiyo kutangaza mabadiliko mengine ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi ameteuliwa kuchukua nafasi yake ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo 




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com