Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANAHABARI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA



Mkufunzi,Peter Kimath akifafanua jambo katika mafunzo ya usalama wa wanahabari

****

Waandishi wa habari wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria ili kuepuka kuingia kwenye migogoro wakati wa kuripoti habari kuelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu Oktoba 2025.


Peter Kimath,Elizabeth Tanzania na Peter Laurence ni wakufunzi waliojengewa uwezo na UTPC kwa kushirikiana na JamiiAfrica, IMS kwa lengo la kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari sanjari na usalama mtandaoni na masuala ya saikolojia ya maisha kwa waandishi wa habari.


Peter Kimath amesema msingi bora wa mwandishi kufanya kazi zake vizuri bila kuingia kwenye changamoto ni kufuata sheria zinazomuongoza,kufuata sheria za nchi na kuangalia sera za chombo anachofanyia kazi kwa lengo la kulisha walaji wake kile wanachotegemea.


“Tunapaswa kuelewa sheria na kanuni zinazohusu uchaguzi na vyombo vya habari, kama Sheria ya Huduma za Habari (2016), Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015) na Kanuni za Tume ya Uchaguzi.”,anasema Kimath.


Mwandishi Nguli,Halfan Diyu anasema mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwani yamewakumbusha vitu vingi muhimu vya kuzingatia wakati wa kuripori habari za uchaguzi na nyingine katika jamii.

“Tunaishukuru UTPCna IMS kwa kuona umuhimu wa mafunzo haya kwetu,naamini tutayatumia vizuri katika kuripoti habari,na kufuata maadili ya kiuandishi ili kuepuka kuingia kwenye msigano".

Mwandishi Hamida Sharifu anasema kutokana na teknolojia vitu vinabadilika kila siku katika tasnia ya habari,hivyo wanahabari wanapaswa kukumbushwa kila wakati katika masuala mbalimbali ikiwemo ulinzi wa taarifa binafsi na sheria zinazowaongoza.

“Nimejifunza vitu vizuri vitakavyonisaidia katika utendaji wangu wa kazi kila siku ikiwemo,namna ya kulinda vifaa vyangu vya kazi,kujilinda wakati wa kuripoti habari uchunguzi,UTPC nawaomba kuendelea kutoa mafunzo kama haya kwani bado wanahabari tunachangamoto nyingi zinahitaji kutatuliwa kwa njia ya kupewa elimu.
Mwandishi Nguli,Halfan Diyu akichangia mada katika mafunzo ya usalama wa wanahabari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com