
Na Woinde Shizza,Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha kimetangaza rasmi majina ya wagombea wake wa nafasi za udiwani kwa Jimbo la Arusha Mjini, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba mwaka huu, huku jina la msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Abdulazizi Chende ‘Dogo Janja’ likivuta hisia za wengi.
Akitangaza majina hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM, Saipurani Ramsey alisema uteuzi huo umezingatia vigezo mbalimbali vikiwemo historia ya uaminifu kwa chama, ushiriki hai katika shughuli za kijamii, ushindi kwenye kura za maoni, pamoja na uwezo wa kushirikiana na wananchi na viongozi.
“Tumefanya mchujo wa kina kuhakikisha tunapata wagombea wenye maadili, uadilifu na uwezo wa kutekeleza majukumu ya udiwani kwa ufanisi,” amesema Ramsey.
Miongoni mwa majina yaliyotangazwa, Abdulazizi Chende (Dogo Janja) ameteuliwa kugombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Ngarenaro, hatua inayotajwa kuleta upepo mpya katika medani ya siasa za Arusha Mjini.
Ramsey amewataka wagombea wote kutumia kampeni zao kuhamasisha mshikamano na maendeleo ya jamii, badala ya kugawa wananchi kwa misingi ya kisiasa.
Hii ndiyo Orodha ya Wagombea Wateule wa Jimbo la Arusha Mjini
Engutoto: Hamza Juma
Moivaro: Philemon Mollel
Levolosi: Abbas Mustafa
Themi: Melace Kinabo
Terat: Julias Sekeyani
Ngarenaro: Abdulazizi Chende (Dogo Janja)
Olorien: Zacharia Mollel
Kati: Abdulrasul Tojo
Osunyai: Elirehema Nnko
Kaloleni: Maximilian Iranghe
Sekei: Emanuel Kisira
Lemara: Matuyani Laizer
Unga-Limited: Mahamudu Omari
Sokoni One: Muksini Juma
Sombetini: Godfrey Kitomari
Sinoni: Peter Inyasi
Olmoti: Robert Komani
Moshono: Siriel Mbise
Eleray: Losioki Laizer
Kimandolu: Abrahamu Mollel
Muriet: Credo Kifukwe
Baraa: Jacob Mollel
Daraja Mbili: Prosper Msofe
Sakina: Hillar Mollel
Social Plugin