.jpeg)
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama kimetangaza matokeo ya kura za maoni kwa ajili ya kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ambapo Benjamin Lukubha Ngayiwa ameibuka kidedea.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga amesema jumla ya kura 6,195 zilipigwa, kura halali zikiwa 6,045 huku kura zilizoharibika zikiwa 80.
Ngayiwa ameongoza kwa kupata kura 2,093, akiwashinda wagombea wenzake akiwemo Sweetbert Charles Nkuba aliyepata kura 1,389 na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa awamu kadhaa, Jumanne Kibela Kishimba aliyepata kura 1,144.
Wengine ni Francis Fikili Mihayo (821), Juliana Kajala Pallangyo (256), James Daudi Lembeli (219) na David Anyandwile Kilala aliyepata kura 191.
Social Plugin