Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MADAHA CHABBA MGOMBEA UBUNGE KISHAPU: KIONGOZI MWENYE DIRA NA UTUMISHI WA UMMA KWA MOYO

Katika zama ambazo jamii inahitaji viongozi wenye maono, uadilifu, na uzalendo wa kweli, jina la Madaha Mayega Chabba linaibuka kama mfano wa kuigwa wa uongozi unaozingatia maendeleo jumuishi ya watu. 

Chabba ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopitishwa kugombea ubunge Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga.

Akiwa na tajriba ya zaidi ya miaka 25 katika sekta ya fedha na benki, Chabba amejijengea heshima kama mtaalamu aliyebobea katika usimamizi, ufanisi wa gharama, na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi yenye tija kwa wananchi wa kawaida.

Anayeitwa na wengi kama "kiongozi mwenye roho ya wananchi", Madaha Chabba sasa ameweka wazi dhamira yake ya kugombea ubunge ili kuwatumikia wananchi kwa kiwango kipya cha ufanisi, uwazi, na uchapakazi. 

Maono yake makubwa ni kuona jamii yenye usawa wa kijamii, ujumuishaji wa kifedha, na fursa kwa vijana na wanawake.

🏛️ Uongozi na Uzoefu wa Kiutendaji

Chabba amehudumu katika nyadhifa mbalimbali za juu ndani ya benki ya CRDB, ikiwa ni pamoja na:

1. Mkuu wa Malipo na Udhibiti – aliongoza mabadiliko ya mfumo wa malipo kitaifa, akihakikisha uwazi na ufanisi.

2. Meneja wa Malipo na Uzingatiaji-  alianzisha kitengo maalum kilichopunguza gharama za uendeshaji kwa kiasi kikubwa.

3. Mdhibiti wa Tawi la Waterfront - alihakikisha huduma bora kwa wateja na uzingatiaji wa viwango vya kitaasisi.

4. Afisa Mikopo  Singida - alifufua tawi lililokuwa likipata hasara kuwa miongoni mwa matawi bora kwa faida na huduma kwa jamii.

🎓 ELIMU NA MAFUNZO YA UONGOZI

Chabba ni Mtaalamu wa benki aliyeidhinishwa (TIOB), mwenye elimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mafunzo ya uongozi wa juu kutoka taasisi mbalimbali barani Afrika, zikiwemo Strathmore University (Kenya) na University of Cape Town (Afrika Kusini). Mafunzo hayo yamemwezesha kuwa kiongozi anayezingatia thamani ya fedha, mbinu za kisasa, na maendeleo shirikishi.

🏅 TUZO NA UTAMBUZI

Ufanisi wa Chabba si wa kuhadithiwa tu, bali umetambuliwa rasmi na taasisi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

 -Tuzo ya Utendaji Bora (2005) Kwa kuleta mabadiliko ya kweli katika huduma za benki.

- Utambuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB (2019) Kwa kuokoa mamilioni ya gharama za uendeshaji.

- Heshima kutoka Halmashauri ya Kishapu (2025)  Kwa kushiriki na kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo Vijijini.

.    Kutambuliwa na CCM na Jumuiya zake (2024/25)  Kwa kujitolea kusaidia ujenzi na shughuli za chama.

🌍 Dira ya Maendeleo

   Chabba anasimama imara katika kupigania:

-Uwezeshaji wa vijana na wanawake

-Uwajibikaji wa taasisi za umma

-Mageuzi ya kiuchumi ya vijiji na miji

-Elimu bora na ujumuishaji wa kijamii

📍 ASILI NA MAISHA YA AWALI

Alizaliwa Mwaka  1971 katika Kijiji cha Kiloleli, Kishapu, Shinyanga Ni zao la Shule za Msingi na Sekondari Mkoani humo, akiwa mfano wa mafanikio kwa kijana wa Kijijini aliyejikwamua kwa bidii, hekima na maono makubwa.

KAULI MBIU YAKE NI: "MANENO KIDOGO MAENDELEO ZAIDI"



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com