Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa, leo Jumanne Julai 1, 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Eunice ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Jiolojia akijikita zaidi kwenye sekta ya Madini, Mafuta na Gesi, amewasili katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa lengo la kujiorodhesha rasmi kwenye kinyang’anyiro hicho kinachovutia wagombea mbalimbali.
Hii si mara ya kwanza kwa Eunice kutia nia ya kuwania nafasi hiyo, kwani mwaka 2020 pia aliomba ridhaa ya chama kugombea ubunge katika jimbo hilo, jambo linaloonesha dhamira yake ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Shinyanga Mjini.
Social Plugin