Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MASELE APENYA MCHUJO CCM! KAMATI KUU YAMPA TIKETI KUISAKA NAFASI YA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, imempitisha aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament), Naibu Waziri Nishati na Madini, na Mbunge wa zamani wa Shinyanga Mjini (2010–2020), Stephen Julius Masele, kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia mchakato wa ndani ya chama hicho.

Katika mchakato huo wa ndani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Masele atachuana na wagombea wengine waliopitishwa ambao ni Mhe. Patrobas Katambi (Mbunge anayemaliza muda wake na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulamhafiz Mukadam, Eustard Athanace Ngatale, Hassan Athuman Fatiu, Hosea Muza Karume, na Paul Joseph Blandy.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hivi karibuni, Masele alisema amerudi na ari mpya ya kuimarisha mshikamano, kurudisha matumaini na kufanikisha maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Shinyanga Mjini.

“Nimelelewa katika misingi imara ya chama na nina rekodi safi ya uongozi. Shinyanga inahitaji kiongozi mwenye uzoefu. Nataka nirudishe furaha iliyotoweka,” alisema kwa msisitizo.

“Mwaka huu tunaandika upya historia. Niko tayari kuwatumikia tena wananchi wangu kwa bidii, heshima, na matokeo yanayoonekana,” alisema Masele.

Uzoefu na Rekodi ya Uongozi

Stephen Masele ni miongoni mwa viongozi wachache nchini wenye uzoefu mpana wa kiuongozi kitaifa na kimataifa.

Amewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).

Pai alihudumu kama Naibu Waziri  wa Nishati na Madini katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,

Alikuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo (2010–2020).

Historia ya Kura za Maoni

Katika uchaguzi wa mwaka 2020, Masele aliibuka kidedea kwenye kura za maoni ndani ya CCM, lakini jina lake halikurudi katika mchujo wa mwisho. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com