Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM YAMTAKA TENA KATAMBI!! YARUDISHA JINA AGOMBEE TENA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa imempitisha Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini katika mchakato wa ndani ya chama.

Katambi sasa anashindana na wagombea wengine waliopitishwa, akiwemo mwanasiasa  Stephen Masele aliyewahi kulitumikia jimbo la Shinyanga Mjini kwa miaka kumi (2010–2020) ambaye pia  amewahi kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Naibu Waziri wa Nishati na Madini.

Wagombea wengine ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulamhafiz Mukadam, Eustard Athanace Ngatale, Hassan Athuman Fatiu, Hosea Muza Karume na Paul Joseph Blandy, katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM atakayewakilisha chama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Mhe. Patrobas Katambi ni Mbunge wa Shinyanga Mjini anayemaliza muda wake wa sasa. Katika kipindi chake cha miaka mitano amejitahidi kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo katika jimbo hilo kwa kushirikiana na serikali na wananchi.

Akichukua fomu ya kuomba uteuzi tena, Katambi alisema,
"Katika miaka mitano tumefanikisha mambo makubwa ambayo yamebadilisha sura ya Shinyanga na kuifanya kuwa jinsi mnavyoiona leo."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com