Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MBONI AMWAPISHA MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FRANK NKINGA

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kutoka ofisini na badala yake waende vijijini kusikiliza na kutatua kero za wananchi wanaowaongoza sambamba na kusimamia ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoendelea na serikali ili iweze kukamilika kwa wakati.

Agizo hilo limetolewa leo Julai 1,2025 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita wakati akimwapisha Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda ambaye aliyeteuliwa Juni 23,2025 na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amewataka kwenda kusikiliza kero za wananchi.

Pia ametoa maagizo kwa Wakuu wa wilaya wote wa Mkoani Shinyanga waendelee kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Mkinda, ameahidi kutekeleza maagizo yote aliyopewa, huku akiahidi kudumisha amani na utulivu katika wilaya hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com