
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Ahmed Ally Salum kugombea tena nafasi ya ubunge katika Jimbo la Solwa, mkoani Shinyanga katika mchakato wa ndani ya chama.
Katika hatua hiyo ya awali ya mchakato wa ndani, Ahmed Salum atachuana na wagombea wengine sita waliochujwa na kupitishwa na CCM ambao ni Sosthenes Julius Katwa, Selemani Emmanuel Choka, Zinguji Mayala Machwele,Leonard Nduta Lukanya, Alphistone Michael Bushi na Costantine Joseph Budaga.



Social Plugin