Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TIP YAENDESHA MAFUNZO YA KUPINGA UKATILI KWA VIONGOZI WA DINI,WALIMU NA VIONGOZI WA MILA KISHAPU


Mratibu wa mradi wa "Chaguo langu haki yangu" unaotekelezwa na TIP kwa kushirikiana na UNFPA na HelpAge Kassim Ngabow  akizungumza kwenye mafunzo ya kuzuia ukatili wa kijinsia Wilayani Kishapu 

Na Sumai Salum - Kishapu

Katika jitihada za kupambana na ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, ukeketaji na mila kandamizi zinazowakandamiza wanawake na watoto,Muungano wa Taasisi za kidini Tanzanzi TIP umefanya mafunzo maalum kwa kushirikisha viongozi wa dini, waalimu wa madrasa na shule ya jumapili pamoja na viongozi wa kimila kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mafunzo hayo muhimu yamefanyika Juni 17, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, yakilenga kutoa elimu ya kina na kuongeza uelewa kwa viongozi kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na umuhimu wa kushirikiana katika kutokomeza kabisa vitendo hivyo katika jamii.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka ofisi ya Maendeleo ya jamii Kishapu Bernadetha Bagenzi amewahimiza washiriki kuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii zao kuhusu madhara ya mila potofu na ukatili wa aina zote.

“Tunawategemea nyinyi kama mabalozi wa mabadiliko kwenye jamii Kwani mna nafasi ya kipekee kuelimisha, kushawishi na kuongoza mabadiliko ya kweli hivyo tukishirikiana, tunaweza kuufuta ukatili wa kijinsia katika kizazi hiki,” amesema Bagenzi.

Mwezeshaji wa mada ya pili iliyohusu mila potovu,mila kandamizi na tamaduni hasi kutoka shirika la TIP Abiduna Ally amesema iko nafasi kubwa ya imani katika kuleta mabadiliko ya kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto nchini kwani mtu akibadilika na kuacha uovu akimtegemea Mungu hawezi kufanya ukatili kulingana na maagizo ya Neno la Mungu pekee.

Mratibu wa mradi wa "Chaguo langu haki yangu" unaotekelezwa na TIP kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi na haki ya kijinsia (UNFPA) na Shirika linalohudumia wazee Tanzania (HelpAge) Kassim Ngabow amesema TIP imepanga kufanya mafunzo hayo kwa viongozi wa dini yatakayowajengea uwezo juu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Halamashauri hiyo.

Mafunzo hayo yametoa fursa ya mjadala mpana ambapo washiriki wamejadiliana, kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo juu ya mbinu bora za kupambana na mila zinazokandamiza wanawake na watoto wa kike.

Aidha, mkutano huo ulimalizika kwa kutungwa kwa maazimio na mikakati ya pamoja, ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii kuanzia majumbani kwao, jamii inayowazunguka, kupitia mimbari za dini na mikutano ya kijamii.

Samabamba na hayo wameazamia kuelimisha jamii kupata uelewa wa pamoja wa kutoa taarifa za matukio ya ukatili kwa vyombo vya dola pamoja na kushirikiana na serikali na mashirika mengine katika mapambano dhidi ya mila kandamizi.
Mwezeshaji wa mafunzo kutoka ofisi ya Maendeleo ya jamii Kishapu Mkoani Shinyanga Bernadetha Bagenzi akizungumza kwenye mafunzo yaliyowakutanisha viongozi wa dini,walimu na viongozi wa mila kuhusu ukatili wa kijinsia Juni 17,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo
Katibu wa Bakwata Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Athuman Ally akizungunza kwenye mafunzo hayo ya kupinga ukatili yaliyoratibiwa na TIP na kufanyika Juni 17,2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Kishapu
Mwezeshaji wa mafunzo mada ya pili iliyohusu mila potovu,mila kandamizi na tamaduni hasi kutoka Shirika la TIP Abiduna Ally akielezea nafasi ya imani katika kuleta mabadiliko ya kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto Juni 17,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com