Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DED KISHAPU AHIMIZA UIMARISHAJI USHIRIKIANO KATI YA NGO's NA SERIKALI


Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Na Sumai Salum - Kishapu

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imeyakutanisha Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali 16 (NGOs) yanayofanya kazi mbalimbali za kijamii Wilayani humo na Uongozi wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili shughuli wanazozifanya katika maeneo yao ya kazi, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili.

Akizungumza katika kikao hicho wakati wa ufunguzi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson ameyapongeza mashirika hayo kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusaidia jamii kwenye afua mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo afya,maji,elimu,miundombinu, jinsia, mazingira na haki za watoto.

Johnson Amesisitiza umuhimu wa kuongea kuimarisha mahusiano ya ushirikiano baina ya mashirika hayo na ofisi za umma ambazo zitawasaidia kuwaeleza kuhusu sheria za nchi na na sera za kisekta zielekezavyo kwani hiyo itasaidia katika utekelezaji wa shughuli zao kuleta matokeo chanya zaidi.

“Tunatambua mchango wenu katika maendeleo ya wananchi wa Kishapu hivyo ni muhimu sana kushirikiana kwa karibu, kubadilishana taarifa, na kupanga kwa pamoja ili tuongeze tija.Pia nawahimiza mkipata nafasi ya fedha zaidi mpanue wigo wa miradi yenu ifike kwenye Kata na Vijiji ambavyo bado havijafikiwa na miradi hii muhimu na elimu iletayo mabadiliko ya kimtazamo” amesema Mkurugenzi Johnson.

Mwakilishi wa Mkuuu wa Wilaya ambaye pia ni Afisa Tawala Fadhiri Mvanga amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika hayo bega kwa bega ili kuleta mabadiliko kwa wananchi na amehimiza kuendelea kutoa elimu ya kujikwamua kiuchumi hasa kwa vijana walioko migodini alimarufu "Wabeshi".

"Kuna badhi ya vijana ni wadogo kiumri lakini wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye uchimbaji na wasipate kitu nashauri ikiwezekana muwekeze pia fedha huko ili wapate elimu ya kubuni vyanzo vipya vya biashara na wajipatie kipato na hata wanaojipenyeza kinyume cha shera na taratibu za nchi" ameongeza Mvanga

Ameongeza kuwa iko sababu ya mashirika kutenga bajeti ya majanga na dharula mbalimbali ili pindi yanapotokea yasiathiri moja kwa moja fedha za miradi wanayotekeleza.

Mwenyekiti wa mashirika Wilayani Kishapu (NaCONGO) Venas Chunga Nikombe, amesema mashirika hayo yatatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa ofisi za serikali ngazi zote pamoja na kutekeleza shughuli zao kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria, kanuni, taratibu na pia kuheshimu mila, desturi na utamaduni za jamii wanazozihudumia.

Katika kikao hicho, wawakilishi wa mashirika mbalimbali wamepata fursa ya kueleza shughuli walizotekeleza, maeneo wanayofanyia kazi, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto wanazokutana nazo.

Kwa upande wao, baadhi ya wawakilishi wa mashirika hayo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya uongozi wa wilaya kuwaita kwa majadiliano ya pamoja, wakisema hatua hiyo ni muhimu kwa uwazi, uelewano na kuimarisha utekelezaji wa miradi kwa tija zaidi.

Maazimio haya yanatarajiwa kuwa msingi wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo endelevu na jumuishi.

Kikao hicho kimejumuisha Mwenyekiti wa mashirika (NaCONGO) ngazi ya Mkoa Bw.Bakari Juma Kibile na miongoni mwa mashirika yaliyoshiriki ni pamoja na KIWOHEDE, TGNP Mtandao, SHIDEPHA+, World Vision, MEDEA, TCRS, baadhi ya wataalamu wa Halmashauri pamoja na viongozi wa mashirika kwa ngazi ya Wilaya.

Kikao hicho kimetajwa kuwa ni mwanzo mzuri wa mpango wa Halmashauri wa kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na uratibu wa pamoja baina ya Serikali na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta matokeo yenye tija kwa wananchi wa Kishapu.



Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Afisa Tawala Fadhiri Mvanga akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Afisa maendeleo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.


Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Shinyanga (NaCONGO) Bakari Juma Kibile akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya kiserikali Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga (NaCONGO) Venas Chunga Jikombe akisoma risala ya mashirika kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com