Mbunge wa jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amechukua fomu ya maombi ya kugombea tena nafasi ya ubunge kwa kipindi kingine cha 2025/30 kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo vyombo vya habari vilivyokuwepo katika eneo la tukio walipotaka mahojiano hakuwa tayari kuzungumzia chochote zaidi alisema wakati ukifika atazungumza.
Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Ruhoro ni miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa kwa wananchi wa jimbo lake kwani wananchi hao wamekuwa wakimchangia fedha kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea tena katika kipindi kingine 2025-2030.


Social Plugin