Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WANACHAMA 67 WA CHADEMA WAHAMIA CCM BAADA YA EVANCE KAMENGE KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE MISENYI

Sehemu ya wanachama wa CHADEMA wakipokelewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Missenyi Bakari Mwacha (mwenye shati la kijani)
Mtia nia ubunge Jimbo la Missenyi Evance Kamenge 


Na Mbuke Shilagi Kagera.

Wanachama 67 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Missenyi wamehamia chama Cha Mapinduzi CCM huku wakisema sababu kubwa ni mtia nia ngazi ya ubunge Evance Kamenge kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Missenyi.

Akiwapokea wanachama hao leo Juni 29,2025 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Missenyi Bakari Mwacha amekiri kuwapokea wanachama 22 Kutoka sehemu mbalimbali katika Jimbo la Missenyi na kwamba watasajiliwa kwa mfumo wa elektronik kwa utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi huku akisema kuwa ataendelea kuwapokea wote mpaka idadi yote itakapo kamilika.


Baadhi ya Wanachama hao akiwemo Remigius Daniel Kamzola aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya Mabale na Apolinary Joseph Kaijage pia Halima John ambao walikuwa wanachama wa CHADEMA wameeleza sababu yao ambayo imepelekea wao kuhama Chama hicho na kuingia CCM kwamba ni Maendeleo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia kijana mpambanaji, mchumi na mkulima Evance Kamenge kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo jambo ambalo wanaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com