
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jovina Japheth ameonesha dhamira ya dhati ya kulitumikia taifa kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kugombea nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kwa wanawake kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Jovina amechukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Mkoa wa Shinyanga kwa kufuata taratibu za chama, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ndani ya chama unaolenga kupata wagombea watakaowakilisha kikamilifu maslahi ya wanawake na wananchi kwa ujumla katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Social Plugin