Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Damas Ndumbaro, amechukua fomu ya kutetea kiti chake tena katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Katika hatua hiyo Ndumbaro ameambatana na mkewe, Bi. Frola Mdima, ofisi ya CCM wilaya, ambapo Katibu wa CCM wilaya, James Mgego, amemkabidhi fomu.
Ndumbaro amesisitiza kuwa kinachomchochea kurudi kwake ulingoni ni kuendeleza miradi ya maendeleo aliyoianzisha kipindi chake cha kwanza, ukiwemo ujenzi wa madarasa 244 yenye thamani ya shilingi bilioni 5.234 pamoja na madawati, meza na viti
Pia ameanzisha mashindano ya "Ndumbaro Cup" akiwa amewagawia vijana mipira 96 na jezi 96, ili kuwachochea kushiriki michezo, kukuza afya, nidhamu na vipaji .
Aidha, huduma za msaada wa kisheria zimeanzishwa chini ya kampeni ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kutoa ushauri bila malipo kuhusu ndoa, ardhi na urithi .
Akiangazia mchango wake katika sekta ya afya,ambayo iligharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.735
pia Ndumbaro alijenga vituo vya afya vinne na zahanati nne na Hospitali ya Rufaa moja
Ndumbaro pia alikabidhi vifaa tiba muhimu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma Desemba 2024, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kupunguza muda wa wagonjwa hospitalini na kuboresha huduma za physiotherapy .
Alisimamia ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Songea, akisisitiza umuhimu wa ubora na ukamilifu wa mradi huo ili kuwapatia wananchi huduma bora kwa wakati .
Vivyo hivyo, kupitia juhudi zake za ubia na serikali, mradi wa maji ulioteuliwa na Rais Samia Suluhu uliwezesha mradi wa maji kukamilika mjini Songea, kwa gharama ya TZS bilioni 145.8, mradi ulioleta usambazaji wa maji safi kwa mamia ya kaya .
Social Plugin