Na Barnabas kisengi Mpwapwa
Ikiwa ni siku ya kwanza kwa kufunguliwa kwa dirisha la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi ya ubunge na udiwani kwa kupitia Chama cha Mapinduzi CCM baadhi ya watia nia wameanza kujitokeza kuchukua fomu za Chama cha Mapinduzi wilaya mpwapwa Mkoani Dodoma
Katika ofisi za chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Njamasii Chiwanga amechukuwa fomu ya kugombea nafasi ya ubunge kupitia chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Mpwapwa mkoani Dodoma
Akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya kugombea ubunge kupitia kura za maoni za chama cha Mapinduzi Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mpwapwa Denes Luhende amemkabidhi fomu ya nafasi ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama cha Mapinduzi amesema fomu hiyo inajieleza vizuri na ina maelekezo yote hivyo ukaijaze kwa umakini na kuirejeaha kama inavyo jielekeza.
Kwa upande wa mtia nia kwa nafasi ya ubunge Jimbo la Mpwapwa Ndugu Njamasii Chiwanga amesema amejipima na kuona anatosha kuweza kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama cha Mapinduzi.
"Nilijitafakari kwa umakini sana na kuona nina uwezo wa kushika hii nafasi ya ubunge kwa kupitia chama changu cha Mapinduzi hivyo leo June 28 2025 nimewiwa kuchukua fomu hii hivyo kwakuwa Chama cha Mapinduzi kina utaratibu wa vikao vyake hivyo baada ya kuchukuwa fomu hii na kurudisha nitasubiri taratibu za chama kama zilivyo"
Zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi za ubunge na udiwa kupitia chama cha Mapinduzi CCM limezinduliwa rasmi leo june 28 2025 na litahitimishwa Julia 2 2025.
Social Plugin