
Katika hali ya kutatanisha, wanawake wawili katika mji wa Pwani, Aisha Wanjiru na Ivana Wangui, wameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuzua tafrani kuhusu mwanaume mmoja aitwaye Wisdom Mwaniki
.Tukio hilo ambalo limesababisha mji huo kugubikwa na minong’ono, lilijiri katikati ya eneo la soko hilo lenye shughuli nyingi na kuvuta umati mkubwa wa watu.
Wisdom Mwaniki ambaye ndiye muhusika mkuu wa mzozo huo ni mtu maarufu sana eneo hilo, watu wengi hasa kina dada wamekuwa wakieleza kuvutiwa naye kwa madai ni mtu mwenye ucheshi sana.
Social Plugin