Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

REA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA KITAIFA YA NISHATI JADIDIFU


-Elimu ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia yaendelea kutolewa

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unashiriki maadhimisho ya Kitaifa ya Nishati Jadidifu yanayoratibiwa na Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu Tanzania (TAREA).

Kaulimbiu ya Maadhimisho haya ni 'Kuwezesha Uendelevu: Kukuza Matumizi ya Nishati Jadidifu’

Katika maadhimisho haya, REA imepata fursa ya kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia sambamba na kushiriki katika mijadala mbalimbali kuhusu nafasi ya nishati jadidifu katika kufikia lengo la Taifa la kufikia 80% ya wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com