Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LISHE KWANZA! RC TELACK AONGOZA MAPAMBANO DHIDI YA UTAPIAMLO LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali Mkoani Lindi akizungumza katika kikao cha Kamati ya Lishe ngazi ya Mkoa

Na Regina Ndumbaro-Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bi Zainab Telack, ameongoza kikao cha Kamati ya Lishe ngazi ya Mkoa kilichofanyika leo tarehe 3 Mei 2025. 

Kikao hicho kimelenga kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024 na Januari hadi Machi 2025. 

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi.

Katika kikao hicho, viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa lishe wamehudhuria kwa lengo la kufanya tathmini na kuweka mikakati mipya ya kuboresha hali ya lishe mkoani humo. 

Kikao kimetoa fursa ya kuwasilisha taarifa kutoka wilaya zote za mkoa wa Lindi ili kuonesha mafanikio, changamoto na mapendekezo ya utekelezaji wa afua za lishe.

Bi Telack kabla ya kufungua rasmi kikao hicho, amepata nafasi ya kuzungumza na viongozi wanaosimamia afya na lishe mkoani humo. 

Katika hotuba yake, amesisitiza umuhimu wa kuwa na mfumo madhubuti wa ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya lishe.

Aidha, amehimiza ushirikiano baina ya wadau wote ili kuhakikisha malengo ya kuboresha hali ya lishe kwa watoto na makundi mengine yaliyo hatarini yanafikiwa. 

Amesisitiza pia kuwa ufanisi wa utekelezaji wa afua hizo utategemea zaidi ushirikiano thabiti, mipango madhubuti na ufuatiliaji wa karibu wa shughuli za lishe katika ngazi zote.



Baadhi ya viongozi wa Serikali Mkoani Lindi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mhe. Zainab Telack katika kikao cha Kamati ya Lishe ngazi ya Mkoa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com