Na Lydia Lugakila _ Bukoba
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amefungua kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe ngazi ya jamii cha robo ya tatu 2024/2025.
Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 09,2025 katika ukumbi wa makao makuu ya halmashauri kikihusisha waganga wafawidhi,afisa lishe na watendaji wa kata.
Akifungua kikao hicho, Mhe. Sima amepongeza juhudi za shule mbalimbali kupanda miti ya matunda na bustani za mboga mboga ili kuimarisha lishe kwa wanafunzi.
Aidha Mhe. Sima ameongeza kuwa kuna baadhi ya vitu ambavyo vinawashusha kwenye asilimia za lishe ikiwemo suala la utapiamlo kwa baadhi ya kata na kutaka vitafutiwe suluhu ya kudumu.
"Lazima tupige vita lishe duni katika Halmashauri yetu,kwa kuzingatia viashiria vyote vya lishe ikiwemo utoaji wa chakula mashuleni kwa asilimia 100",amesema.
Naye afisa lishe Bi.Janeth Mahona ameeleza mafanikio ya afua za lishe kwa robo ya tatu ikiwemo kuongezeka kwa mashine 3 za kurutubisha unga kata ya kemondo,kufanyika kwa mafunzo wezeshi ya matibabu ya utapiamlo,kufanyika kwa matibabu ya utapiamlo kwa watoto 6 katika hospitali ya wilaya,mafunzo juu ya uchakataji wa soya kwa kina mama 49 na kuendeleza vitalu vya lishe shuleni.
Bi. Janeth ameongeza pamoja na mafanikio hayo kumekua na changamoto kadhaa ikiwemo ucheleweshwaji wa taarifa za lishe kwa baadhi ya kata na baadhi ya wanafunzi kutokula chakula shuleni.

Social Plugin