
Na Regina Ndumbaro _ Ruvuma
Mbunge wa Jimbo la Madaba, Dkt. Joseph Kizito Mhagama, amepata pongezi kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Uss, kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
Ismail ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya mwenge katika jimbo hilo, akisema kuwa Dkt. Mhagama ameendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa namna anavyowasilisha na kusimamia masuala ya wananchi bungeni.
Katika hotuba yake, Ismail ameeleza kuwa mchango wa Mbunge huyo katika maendeleo ya jimbo lake unaonekana wazi kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
Amebainisha kuwa dhamira ya dhati ya Dkt. Mhagama katika kuboresha maisha ya wananchi wake ni ishara ya uongozi wa kizalendo unaojali maslahi ya wananchi.
Mbali na pongezi hizo, Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge ametoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Madaba kuendelea kumuunga mkono mbunge wao, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Amesisitiza kuwa uaminifu na mshikamano wa wananchi ndio msingi wa kuendeleza kasi ya maendeleo yaliyoanzishwa
Wananchi wa Madaba wameonekana kufurahishwa na kauli hiyo, wakieleza kuwa Dkt. Mhagama amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo, hususan katika sekta za afya, elimu na miundombinu.
Wamesema wako tayari kuendelea kushirikiana naye na kumuunga mkono katika jitihada zake za kuwaletea maendeleo endelevu.



Social Plugin