Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza na Shinyanga, wametembelea miradi mbalimbali ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika Jiji la Mwanza, ikiwa ni sehemu ya ziara iliyoandaliwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali.
Ziara hiyo imefanyika leo Mei 2, 2025, ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, kwa lengo la kuwawezesha waandishi hao kushuhudia kwa macho hatua za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Miradi waliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa vivuko vipya vitano, daraja la Kigongo -Busisi, pamoja na meli mpya kubwa ya MV Mwanza, ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Msigwa amesema miradi hiyo inalenga kuondoa changamoto za usafiri na usafirishaji katika ukanda wa Ziwa Victoria, sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.
“Miradi hii ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kuleta maendeleo ya kweli na ya haraka kwa wananchi. Tunataka wananchi wote wajue kinachoendelea na wawe sehemu ya mafanikio haya,” amesema Msigwa.
Waandishi wa habari wamepata fursa ya kutembelea maeneo ya ujenzi, kuuliza maswali kwa wahandisi na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo, pamoja na kujionea namna Serikali inavyosimamia kwa karibu miradi hiyo mikubwa ya kimkakati.
Hatua hizi ni uthibitisho wa dhamira thabiti ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupeleka huduma bora karibu na wananchi, huku miradi mingi ikitekelezwa kwa wakati na kwa viwango vya kimataifa. Kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa nchini inatoa matumaini makubwa kwa Watanzania kuhusu mustakabali wa maendeleo ya Taifa.
Serikali imeendelea kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika kwa namna inavyoweka kipaumbele katika miundombinu, uchumi jumuishi na uwazi kwa wananchi. Miradi kama hii si tu kwamba inarahisisha maisha ya kila siku, bali pia inatoa ajira, kukuza biashara, na kuimarisha mshikamano wa kitaifa kupitia maendeleo shirikishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakiwa katika Meli Mpya ya MV Mwanza - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waandishi wa habari wakiwa katika Meli Mpya ya MV Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakiwa katika Meli Mpya ya MV Mwanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Daraja na Kigongo - Busisi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Vivuko vitano vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa na waandishi wa habari wakitembelea Vivuko vinavyojengwa Jijini Mwanza
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin